Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 03:08

Wa-Ivory Coast wakimbilia kutoa fedha katika benki


Laurent Gbagbo, Rais wa Ivory Coast asiyetambulika kimataifa huku akikataa kukabidhi madaraka kwa mpinzani wake

Watu wa Ivory Coast wanaharakisha kutoa fedha kutoka kwenye benki, wakati khofu ikiongezeka ya matatizo ya kisiasa nchini humo yatasababisha kuanguka kwa mfumo wake wa benki.

Wateja walipanga mistari mirefu nje ya mabenki, katika mji mkuu wa Abidjan hapo Jumatano, lakini baadhi walionekana hawakuweza kutoa fedha zao zote. Baadhi ya benki zinadhibiti utoaji wa fedha, wakati mashine nyingi za ATM hazikuwa na fedha.

Harakati hizo zilianza wiki hii baada ya benki zisizopungua tatu za BNP Paribas, Citibank na Standard Chartered Bank, walipotangaza walikuwa wanasitisha oparesheni zao huko Ivory Coast, kutokana na matatizo ya kisiasa. Jumatano, soko la hisa la kieneo la Afrika magharibi huko Abidjan, pia lilisitisha oparesheni zake.

Usimamishwaji huo ni pigo la karibuni katika suala la fedha kwa Rais Laurent Gbagbo anayeng’ang’ania madaraka, ambaye anakataa shinikizo la kimataifa la kukabidhi madaraka. Mataifa mengi yanamtambua mpinzani wake Alassane Ouattara kama mshindi wa uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana.

Mwezi uliopita benki kuu ya Afrika Magharibi ilimzuia bwana Gbagbo fursa ya kupata fedha za serikali ikiwa ni juhudi za kumlazimisha ajiuzulu. Iliyaonya mabenki kwamba kufanya biashara na serikali ya Gbagbo kunaweza kupelekea vikwazo. Vikwazo vya uchumi vinamaanisha kuinyima fedha inazohitaji serikali ya Gbagbo ili kuwalipa wanajeshi ambao wanamtii.


XS
SM
MD
LG