Tajani amesema hukumu za kifo dhidi ya watu wanaoshiriki katika maandamano au wanawake ambao wamekaidi kuvaa hijabu ni aina ya adhabu ya kupita kiasi na isiyokubalika.
Amesema “Kuvua hijabu au kushiriki katika maandamano sio kosa ambalo linaweza kusababisha hukumu ya kifo popote pale duniani.”
Maandamano ya nchi nzima yalizuka miezi mitatu iliyopita baada ya kifo cha mwanamke wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 22, Mahsa Amini kilichotokea akiwa chini ya ulinzi wa polisi, ambaye alikamatwa na polisi wa maadili wakitekeleza sheria za lazima za mavazi za Jamhuri hiyo ya Kiislamu.