Meli ya uokoaji ya Geo Barents, inayoendeshwa na shirika la madaktari wasiokuwa na mpaka MSF, ikiwa na wahamiaji 248, iliwasili Salerno, kusini magharibu mwa Campania.
Meli nyingine ya uokoaji kwa jina Humanity 1, inayoendeshwa na shirika la msaada la SOS, imeruhusiwa na maafisa wa Italy, kuingia katika bandari ya Bari ikiwa na wahamiaji 261.
Meli hizo zilikuwa zinakabiliwa na hali mbaya ya hewa, zikipigwa na mawimbi ya bahari yenye urefu wa mita 3 na upepo mkali.
Hali ya majibizano iliongezeka kati ya Italy na Jirani yake - Ufaransa, mwezi uliopita, baada ya Ufaransa kuruhusu boti yenye wahamiaji ambayo ilikataliwa na Italy.
Maafisa wa Italy wamesema kwamba wameruhusu meli hizo kuingia katika bandari zake kutokana na hali mbaya ya hewa wala sio kwamba imebadilisha sera yake kuhusu wahamiaji.