Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:13

"Itakua vigumu kumaliza vita vya Ukraine" asema waziri wa ulinzi wa Uturuki


Waziri wa ulinizi wa Uturuki akizungumza na waandishi habari mjini Ankara.
Waziri wa ulinizi wa Uturuki akizungumza na waandishi habari mjini Ankara.

Uturuki imekiri Jumamosi kwamba uvamizi wa Russia nchini Ukraine "hautamalizika kwa urahisi," licha ya Ankara kurudia mara kadhaa juhudi za kupanga mazungumzo ya amani kati ya Kyiv na Moscow.

Uturuki ambayo ni mwanachama wa NATO, yenye uhusiano mzuri na pande zote, imejiweka katika hali ya kutopendelea upande wowote na kujaribu kutafuta njia za kusitisha mapigano bila ya kufanikiwa hadi hivi sasa.

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki, Hulusi Makara amewaambia waandishi habari katika mkutano wa mwisho wa mwaka kwamba, licha ya juhudi zote inaonekana vita hivyo vinavyoendelea kwa miezi 10 havitamalizika kwa urahisi.

"Haitokuwa kosa kusema kwamba licha ya nia yetu njema na wito wa kusitisha mapigano, vita hivi vitaendelea hadi mwaka 2023," amesema Akar.

Uturuki ambayo ilisaidia kufikiwa makubaliano pamoja na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuruhusu usafirishaji wa nafaka wa Ukraine kupitia bahari ya Black Sea, wakati wa majira ya joto, inajaribu kuwaleta pamoja viongozi wa Russia na Ukraine kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza vita hivyo.

"Sisi waturuki, tunatoa wito wa kusitisha mapigano, angalau usitishaji mapigano kwa ajili ya huduma za dharura. Hapo tena usitishaji wakudumu wa mapigano na baadae mazungumzo ya Amani," amesema waziri Akar

XS
SM
MD
LG