Taasisi hiyo iitwayo Institute for the Study of War -ISW yenye makao yake mjini Washington ya Utafiti wa Vita ilisema Jumamosi kwamba hakukuwa na maendeleo yeyote yaliyothibitishwa na vikosi vya Russia huko Bakhmut.
Tathmini ya hivi karibuni ya taasisi hiyo ya wasomi kuhusu vita vya muda mrefu zaidi vya ardhini ilisema kwamba vikosi vya Russia na vitengo vya Kundi la Wagner linalodhibitiwa na Kremlin viliendelea kufanya mashambulizi ya ardhini katika mji huo lakini hakuna ushahidi kwamba walikuwa wamesonga mbele.
Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumapili kwamba alimpa cheo cha juu zaidi cha kitaifa, shujaa wa Ukraine mwanajeshi ambaye inadhaniwa aliuwawa na watu wanaozungumza lugha ya Kirussia.
Facebook Forum