Hamas iliishutumu Israel kwa kujaribu kuvuruga makubaliano yaliyopo ya kusitisha mapigano na kusema uamuzi wake wa kusitisha msaada ulikuwa unyang’anyi wa bei nafuu, uhalifu wa kivita na shambulizi la wazi kwenye usitishaji huo, ambao ulifanyika Januari baada ya mazungumzo ya zaidi ya mwaka mmoja.
Awamu ya kwanza ya usitishaji mapigano, ambayo ni pamoja na kuongezeka kwa msaada wa kibinadamu, ilimalizika Jumamosi.
Pande hizo mbili bado hazijafanya mazungumzo ya awamu ya pili, ambapo Hamas ilikuwa iwaachilie mateka kadhaa waliosalia ili kujitoa kwa Israel na kusitisha mapigano ya kudumu.
Forum