Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 18:08

Israel yawaokoa mateka wawili waliokuwa wanashikiliwa na Hamas huko Rafah


Mateka Fernando Simon Marman, kulia na Luis Har kushoto wakiwakumbatia ndugu zao baada ya kuokolewa huko Ukanda wa Gaza walipokuwa wanashikiliwa na Hamas, Februari 12, 2024.
Mateka Fernando Simon Marman, kulia na Luis Har kushoto wakiwakumbatia ndugu zao baada ya kuokolewa huko Ukanda wa Gaza walipokuwa wanashikiliwa na Hamas, Februari 12, 2024.

Israel Jumatatu iliwaokoa mateka wawili waliokuwa wanashikiliwa na wanamgambo wa Hamas huko Rafah, lakini mashambulizi ya anga yaliua Wapalestina 67 katika mji huo wa kusini mwa Gaza ambako watu milioni moja waliohama makazi yao wanaishi kama wakimbizi tangu miezi minne ya mashambulizi ya mabomu.

Jeshi la Israel, idara yake ya upelelezi na kitengo maalum cha polisi walisema waliokoa watu wawili, Fernando Simon Marman mwenye umri wa miaka 60, na Louis Har mwenye umri wa miaka 70, ambao wana uraia pacha wa Israel na Argentina.

Wawili hao walikuwa miongoni mwa mateka 240 walioshikiliwa na Hamas katika shambulio la Oktoba 7 ndani ya Israel ambalo lililua watu 1,200 na kupelelea Israel kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Miezi minne tangu vita kuzuka, maafisa wa afya huko Gaza wanasema zaidi ya Wapalestina 28,000 waliuawa na wengine 68,000 kujeruhiwa.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipongeza kuokolewa kwa mateka hao na kutupilia mbali tuhuma za Jumuia ya kimataifa kuhusu mipango yake ya kufanya mashambulizi ya ardhini ili kutokomeza vikosi vine vya Hamas huko Rafah.

Forum

XS
SM
MD
LG