Israel ilishambulia mamia ya malengo ya Hezbolah Jumatatu kwa mashambulizi ya anga ambayo maafisa wa afya wa Lebanon wanasema yameuwa takriban watu zaidi ya 270 na kufanya kuwa shambulizi lenye mauaji makubwa nchini humo katika karibu mwaka mmoja wa mzozo.
Baada ya mapambano makali ya mpakani tangu mzozo ulipozuka , Israel imewaonya watu kuhama katika maeneo ambayo wamesema kundi lenye silaha lilikuwa linahifadhi silaha.
Karibu mwaka mmoja wa vita dhidi ya Hamas huko Gaza katika mpaka wake wa kusini , Israel inahamisha lengo lake katika mpaka wa kaskazini, ambako kundi la Hezbolah linaloungwa mkono na Iran limekuwa likifyatua roketi nfani ya ISRAEL kumuunga mkono mshirika wake Hamas.
Forum