Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 08:35

Israel yaripoti mashambulizi kwenye mji wa Khan Younis, kusini mwa Gaza


Picha iliochkuliwa kutoka mji wa Rafah ikionyesha moshi ukipaa kwenye anga ya Khan Younis. Februari 26, 2024.
Picha iliochkuliwa kutoka mji wa Rafah ikionyesha moshi ukipaa kwenye anga ya Khan Younis. Februari 26, 2024.

Jeshi la Israel Jumanne limeripoti mshabulizi kwenye mji wa Khan Younis kusini mwa Gaza, wakati maafisa wa Palestina wakisema kwamba mashambulizi ya Israel kwenye eneo hilo hilo, yameua takriban watu 17.

Maafisa wa Palestina wamesema kwamba mashambulizi hayo yamefanyika karibu na hospitali ya European, iliyoko kwenye kitongonji cha Hamad. Jeshi la Israel limesema kwamba lililenga miundombinu ya magaidi huko Hamad, na kwamba limewakamata darzeni ya wanamgambo wa Hamas, pamoja na wapiganaji wa kundi la Islamic Jihad, waliokuwa wamejificha miongoni mwa raia.

Mapigano huko Gaza yangali yanaendelea licha ya shinikizo la sitisho la mapigano, ambalo pia linajadiliwa kwenye mazungmzo yanayoendela Misri. Israel imeyakwepa mazungmzo ya Cairo, wakati ikiilaumu Hamas kwa kutotoa orodha ya majina ya mateka wanaoendelea kushikiliwa huko Gaza.

Afisa wa ngazi ya juu wa Hamas amewaambia wana habari Jumanne kwamba waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ni wa kulaumiwa kutokana na kutofikiwa kwa makubaliano, na kwamba ni jukumu la mshirika wake wa karibu, Marekani, kuhakikisha hilo linafanyika.

Forum

XS
SM
MD
LG