Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 27, 2025 Local time: 07:21

Israel yapinga Marekani kufanya uchunguzi wa mauaji ya mwanahabari


Waziri wa ulinzi wa Israel, Benny Gantz
Waziri wa ulinzi wa Israel, Benny Gantz

Wizara ya sheria ya Marekani imeanzisha uchunguzi wa mauaji ya mwanahabari wa shirika la habari la Aljazeera, Shireen Abu Akleh.

Israel, Jumatatu imethibitisha hatua hiyo, na kuushutumu uchunguzi huo kwa kusema itakuwa ni kosa kubwa na kuapa kutotoa ushirikiano.

Waziri wa ulinzi wa Israel Benny Gantz, alitoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa Twitter, akisema Israel imeweka wazi kwa Marekani kwamba haitotoa ushirikiano wa uchunguzi wowote wa nje.

Amesema hawata ruhusu kuingiliwa katika masuala ya ndani ya Israel.

Mwanahabari wa Kipalestina ambaye alikuwa ana andika habari za oparesheni za Israel ndani ya Palestina, Abu Akleh, alikuwa pia raia wa Marekani.

Msemaji wa wizara ya sheria ya Marekani hakujibu lolote baada ya kuombwa kujibu taarifa ya waziri wa Israel, Gantz.

Haikuwa wazi kuhusu lini hasa uchunguzi huo unaweza kuanza, na kile kitakacho chunguzwa.

Lakini uchunguzi wa Marekani ndani ya Israel imekuwa ni jambo la nadra na linaweza kutikisa uhusiano wa mataifa hayo mawili.

XS
SM
MD
LG