Maafisa wa jeshi la Israel walisema Jumamosi zaidi ya malengo 50 ya Hamas katika eneo la Khan Yunis kusini mwa Gaza yalipigwa na vikosi vya anga, majini na ardhini. Jeshi lilisema lilifanya mashambulizi kaskazini na kwamba zaidi ya malengo 400 huko Gaza yamepigwa tangu mapigano kuanza tena siku mbili zilizopita.
Ghasia za Jumamosi zilikuja siku moja baada ya mashambulizi ya anga ya Israel kwenye eneo la Palestina kuwaua watu 184, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza.
Nchini Syria, Wizara ya Ulinzi ilisema Israel ilifanya mashambulizi ya anga karibu na Damascus mapema Jumamosi. Vyombo vya habari vya serikali ya Syria viliripoti kwamba vyombo vya ulinzi wa kijeshi viliangusha makombora mengi ya Israeli. Ilisema hakuna ripoti za majeruhi.
Forum