Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 11, 2025 Local time: 01:05

Israel yafanya mashambulizi Gaza


Jeshi la Israel, limefanya mashambulizi ya anga na operesheni za ardhini katika Ukanda wa Gaza, Jumatano, huku wapatanishi nchini Misri wakifanyia kazi mpango wa kusitisha mapigano ambao ungesitisha mzozo huo kwa wiki kadhaa.

Jeshi la Israel limeripoti shambulizi la anga katika mji wa Beit Hanoun na kuua wanamgambo wawili waliohusika katika shambulizi la kigaidi la Oktoba 7 dhidi ya Israel.

Mashambulizi mengine ya Israel, yalifanyika katikati mwa Gaza na katika eneo la Khan Younis, katika sehemu ya kusini ya ukanda huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Cameron, amesema anapanga kutoa onyo kwa Israeli, Jumatano kuhusu uhitaji wa kuwezesha misaada zaidi ya kibinadamu kuingia katika Ukanda wa Gaza na kushughulikia kile Cameron, alichokita mateso ya kutisha.

Forum

XS
SM
MD
LG