Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 01:02

Israel: Waziri mpya wa usalama aagiza polisi kuondoa bendera za Palestina kwenye maeneo ya umma


Itamar Ben Gvir, waziri mpya wa usalama wa taifa wa Israel na kiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kulia, akiwasiji mjini Jerusalem kuitembelea soko ya Mahane Yehuda, Disemba 30, 2022. Picha ya AFP

Waziri mpya wa usalama wa taifa wa Israel wa mrengo mkali wa kulia Itamar Ben-Gvir Jumapili amesema aliwaagiza polisi kuondoa bendera za Palestina kwenye maeneo ya umma.

Sheria za Israel haziharamishi bendera za Palestina lakini polisi wana haki ya kuziondoa katika matukio ambapo wanaona kuna tishio kwa usalama wa umma.

Maagizo kutoka kwa Ben-Gvir, ambaye anaongoza chama chenye msimamo mkali katika serikali mpya ya Benjamin Netanyahu na kama waziri anayesimamia polisi, yanaonekana kuchukua msimamo mkali kutaka bendera hizo ziondolewe.

Agizo hilo linafuatia kuachiliwa wiki iliyopita kwa mfungwa wa Kipalestina wa muda mrefu, aliyepatikana na hatia ya kumteka nyara na kumuua mwanajeshi wa Israel mwaka 1983, ambaye alipeperusha bendera ya Palestina akipokelewa kama shujaa katika kijiji chake kaskazini mwa Israel.

Katika taarifa, Ben-Gvir alisema kupeperusha bendera ya Palestina ni kitendo cha kuunga mkono ugaidi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG