Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 18:55

Israel yaishutumu Marekani 'kuunda kundi' lililopitisha azimio la ujenzi wa makazi


Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura kupitisha azimio dhidi ya Israel kwa ujenzi wa makazi.
Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura kupitisha azimio dhidi ya Israel kwa ujenzi wa makazi.

Israeli imeendelea kuishutumu vikali Marekani juu ya uamuzi wake wa kuacha kutumia kura yake ya turufu katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloitaka Israeli kusitisha ujenzi wa makazi.

Ron Dermer, balozi wa Israeli mjini Washington, ameishutumu serikali ya Obama kwa “kuunda genge” la kuikandamiza nchi yake katika kura ya wiki iliyopita.

“Kinacho ghadhibisha ni kuwa Marekani bila ya shaka ilikuwa inalisaidia genge hilo. Nafikiri ilikuwa siku ya majonzi makubwa, na kipindi chenye kuaibisha,” mwanadiplomasia wa Israeli aliiambia CNN Jumatatu.

Jumatatu, Trump amehoji uwezo wa UM, akiita ni klabu ya watu “kuweza kujistarehesha.”

Rais-mteule aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa UM ungetakiwa “kuwa na uwezo mkubwa,” lakini imebakia kuwa “ ni klabu ya watu kukusanyika, kuzungumza na kustarehe. Inasikitisha!”

Siku ya Ijumaa, Trump alionya kuwa, “upande wa UM, mambo yatabadilika ifikapo Januari 20.”

Uamuzi wa serikali ya Obama kuzuia kura ya turufu siku ya Ijumaa, ilitupilia mbali madai ya Trump kwamba Marekani kutotumia kura hiyo kumedhihirisha sintofahamu iliyofikia kileleni kati yake na Israeli.

“Sitisheni shughuli zote za Ujenzi wa makazi”

Siku ya Ijumaa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio likiitaka Israeli kuacha mara moja kusitisha shughuli zote za ujenzi wa makazi yote katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa kimabavu na Israeli, ikiwemo Jerusalem Mashariki.”

Marekani ambayo ina kura ya turufu katika baraza la usalama, ilijizuia kupiga kura hiyo, na kutoa nafasi kuchukuliwa hatua za kupitishwa azimio la kwanza tangu 1979 kuilamu Israel juu ya sera yake ya ujenzi wa makazi.

XS
SM
MD
LG