Lakini alifuta uwezekano wa sitisho la jumla la mapigano katika vita vya mwezi mmoja kati ya Israel na Hamas.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha ABC News, Netanyahu amesema anatarajia Israel “itakuwa na jukumu la jumla la usalama” huko Gaza kwa muda usiojulikana baada ya kufikia lengo lake la kuwaondoa Hamas.
“Wakati hatuna jukumu la usalama, kile tulichonacho ni kuibuka kwa ugaidi wa Hamas kwa kiwango ambacho hatuwezi kukifikiria,” Netanyahu amesema.
White House Jumatatu ilisema kwamba Rais Joe Biden na Netanyahu walijadili kwa njia ya simu uwezekano wa sitisho la mapigano la kimkakati ili kuruhusu raia wa Gaza kuondoka kwa usalama katika maeneo ambayo mapigano yanaendelea, kuhakikisha misaada inawafikia raia wanaohitaji, na jinsi ya kuwezesha kuachiliwa huru kwa mateka.
Forum