Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 10:23

Israel inafanya operesheni katika hospitali ya Shifaa huko Gaza City


Jeshi la Israel limetoa video siku za karibuni ikionyesha mateka katika hospitali ya Shifa.
Jeshi la Israel limetoa video siku za karibuni ikionyesha mateka katika hospitali ya Shifa.

Vikosi vya Israel vinachukua hatua hii kwa sababu maafisa wa Hamas wanaitumia hospitali hiyo kuongoza mashambulizi dhidi ya Israel.

Jeshi la Israel limesema Jumatatu kuwa linafanya operesheni katika hospitali ya Shifa huko Gaza City, eneo ambalo limepata ukosoaji wa kimataifa kwa uvamizi wa mwezi Novemba.

Msemaji wa jeshi la Israel, Admirali Daniel Hagari amesema katika taarifa yake kwamba vikosi vya Israel vinachukua hatua Jumatatu kwa sababu maafisa wa ngazi ya juu wa Hamas wanaitumia hospitali hiyo kuongoza mashambulizi dhidi ya Israel.

Tutafanya operesheni hii kwa tahadhari na uangalifu huku tukihakikisha hospitali inaendelea na kazi yake muhimu, alisema Hagari. Mashahidi waliripoti mashambulizi ya anga katika eneo la hospitali hiyo, ambayo ni kubwa sana katika Ukanda wa Gaza, pamoja na uwepo wa vifaru vya Israeli.

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Joseph Borrell amesema Israel inachochea njaa katika Gaza na inatumia njaa kama silaha ya vita.

Forum

XS
SM
MD
LG