Kwa kutumia lugha ya kiarabu katika kurasa za mitandao ya Facebook na X, Israel imewaambia Wapalestina kwamba kuheshimu amri hiyo ni jambo la usalama kwa maisha yao na familia zao.
Wengi wa Wapalestina wametakiwa kuondoka kaskazini mwa Gaza, mapema katika vita vya miezi miwili na Hamas.
Kutokana na uwezekano wa mashambulizi zaidi katika eneo hilo Israel imewaeleza Wapalestina kuondoka katika maeneo 34 ambayo yote yanapatikana kusini mwa mji wa Khan Younis, na kuelekea katika eneo ambalo limeshajaa kuhifadhi watu ama kile kinachoitwa ukanda wa kibinadamu uliopo Al Mawasi, eneo la kilimo ambalo lipo karibu na bahari ya Mediterranean.
Forum