Riad Malki, amesema katika taarifa kwamba alikuwa anarudi Israel kutoka kwenye hafla ya kuapishwa kwa rais wa Brazil, alipoarifiwa kwamba Israel imefuta hati za kusafiria za maafisa wa ngazi ya juu wa Palestina.
Hati hizo huwa zinawaruhusu maafisa wa Palestina kuingia na kutoka Ukingo wa Magharibi, unaokaliwa kimabavu, kinyume na ilivyo kwa raia wa kawaida wa Palestina.
Hatua hiyo inaashiria msimamo mkali wa serikali ya sasa ya Israel dhidi ya wapalestina, na inajiri wakati ambapo ripoti za machafuko huko Ukingo wa Magharibi zinaongezeka.