Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 20:53

Israel imefanya shambulizi Ukanda wa Gaza na kuwauwa watu wanane


Shambulizi la Israeli eneo la Khan Younis huko kusini mwa Ukanda wa Gaza
Shambulizi la Israeli eneo la Khan Younis huko kusini mwa Ukanda wa Gaza

Mashambulizi hayo yanafuatia siku moja baada ya Israel kuamuru kuondoka  hivi karibuni kwa raia wa Palestina

Wanajeshi wa Israel walifanya mashambulizi leo Jumanne huko kusini mwa Ukanda wa Gaza huku maafisa wa afya wa Palestina wanasema watu wasiopungua wanane waliuawa.

Mashambulizi hayo ni pamoja na mashambulizi ya mabomu ya Khan Younis, siku moja baada ya Israel kuamuru kuondoka hivi karibuni kwa raia wa Palestina. Jeshi la Israel limesema Jumanne kuwa lilifanya mashambulizi ya anga usiku wa kuamkia leo katika eneo la Khan Younis ambako wanamgambo walirusha roketi 20 kuelekea makazi ya walowezi wa Israel.

Mashambulizi zaidi ya anga ya Israel yalilenga mji wa kusini wa Rafah, wakati wanajeshi wa ardhini wa Israel wakifanya operesheni dhidi ya Hamas katikati mwa Gaza, jeshi limesema.

Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaambia waandishi wa habari siku ya Jumatatu kwamba amri ya Israel ya kuondoka kwa wakazi huko Khan Younis inaonyesha hakuna sehemu salama huko Gaza na kwamba juhudi zaidi zinahitaji kufanywa ili kuwalinda raia.

Forum

XS
SM
MD
LG