Waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema kuwa nchi yake imeweka hali ya tahadhari kwenye mji mkuu Jumatatu huku shule zikifungwa kutokana na tishio la shambulizi la kigaidi, baada ya kufanya kikao na baraza la kitaifa la usalama.
Sehemu zingine za nchi pia zimewekwa katika hali ya tahadhari ya kiwango cha tatu. Afisa wa ngazi ya juu amesema vikosi vya usalama nchini humo vimekuwa vikisaka washukiwa wanaohusishwa na shambulizi la karibuni mjini Paris huku wakazi wa Brussels wakishuhudia ongezeko la askari wanaofanya doria kwenye mitaa .
Njia za reli mjini humo zote zimefungwa leo. Waziri wa mambo ya ndani Jan Jambon amesema mamlaka zina msaka mshukiwa wa shambulizi la Paris Salah Abdeslam anaeaminika kuingia Ubelgiji baada ya shambulizi hilo lililouwa watu 130 pamoja na mashambulizi mengine ya nivemba 13 yaliodaiwa kutekelezwa na Islamic State.