Limeonekana kuwa tangazo la kwanza rasmi la kundi hilo kuhusu hatma ya kiongozi wake tangu Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki aliposema mwezi Aprili kwamba maafisa wa ujasusi wa Uturuki walimuua kiongozi huyo wa ISIS nchini Syria.
Kundi hilo lilipata nguvu mwaka 2014 wakati kiongozi wake wa wakati huo, Abu Bakr al-Baghdadi, alipotangaza eneo linalodhibitiwa na kundi hilo kuwa chini ya sheria kali za kiislamu.
Abu Hussein al-Hussein al-Quraishi alichukua uongozi wa ISIS mwezi Novemba mwaka 2022, baada ya mtangulizi wake kuuawa pia nchini Syria.
Forum