Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 15:28

Ireland yaahidi kuhakikisha raia wake anayeshikiliwa Iran anakuwa huru


Raia mwenye asili ya Ufaransa na Ireland, Bernard Phelan, anayeshikiliwa Iran.
Raia mwenye asili ya Ufaransa na Ireland, Bernard Phelan, anayeshikiliwa Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland, Alhamisi amesema serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa raia wa wa asili ya Ufaransa na Ireland anayeshikiliwa Iran anaachiliwa.

Kauli hiyo imetolewa baada ya familia yake kuitaka Dublin kuongeza juhudi za mazungumzo kwa sababu ya wasiwasi wa afya yake kufuatia mgomo wa kula.

Micheal Martin aliuambia mkutano wa waandishi wa habari huko Dublin, kueleza watafanya kila wawezalo kusaidia kumwachilia Bernard Phelan, ambaye ni mshauri wa masuala ya usafiri mwenye umri wa miaka 64 anayeishi Paris.

Phelan ni mmoja wa raia saba wa Ufaransa wanaoshikiliwa na Iran, ambaye alikamatwa mwezi Oktoba alipokuwa akisafiri nchini humo kufuatia maandamano ya hivi karibuni ya kupinga serikali.

XS
SM
MD
LG