Israel imekasirishwa na hatua hiyo na kuwaita mabalozi wake katika nchi hizo kurudi Israel.
Waziri mkuu wa Spain Pedro Sanchez ameitaja hatua hiyo kuwa yenye lengo la kushinkiza kusitishwa vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas huko Gaza.
Israel ilianzisha operesheni ya kijeshi huko Gaza kujibu mashambulizi ya Hamas yaOktoba 7 yaliyoua watu 1200 na kutekwa nyara watu 250.
Kulingana na wizara ya afya ya Gaza, mashambulizi ya Israel katika eneo hilo yameua watu zaidi ya 35,000.
Spain imekuwa ikishawishi mataifa ya Ulaya yakiwemo Ufaransa, Ureno, Ubelgiji na Slovenia kuunga mkono juhudi za kuitambua Palestina kama taifa kamili.
Forum