Taarifa ya serikali ya Iraq imesema Bagdad ilimwita balozi wake mdogo nchini Sweden, na shirika la habari la serikali ya Iraq limeripoti kwamba Iraq ilisitisha kibali cha kufanya kazi kwenye ardhi yake kwa kampuni ya Sweden ya Ericsson.
Waandamanaji wanaopinga Uislamu, mmoja wao ni mhamiaji wa Iraq aliyehamia Sweden ambaye alichoma Qurani nje ya msikiti wa Stockholm mwezi Juni, walikuwa waliwasilisha maombi na kupewa ruhusa na polisi wa Sweden kuchoma Qurani nje ya ubalozi wa Iraq jana Alhamisi.
Katika tukio hilo, waandamanaji walipiga teke na kuharibu kwa kiasi fulani kitabu ambacho walisema ni Qurani lakini waliondoka eneo hilo baada ya saa moja bila kukichoma moto.
Waziri wa mambo ya nje wa Sweden Tobias Billstrom amesema wafanyakazi kwenye ubalozi wa Sweden mjini Bagdad wako salama lakini maafisa wa Iraq walishindwa kutekeleza wajibu wao wa kuulinda ubalozi.
Forum