Waziri mkuu Adel Abdul-Mahdi alitangaza marufuku ya kutembea nje kama namna ya kudhibiti maandamano hayo katika mji mkuu na maeneo mengine ya nchi.
Tangu maandamano hayo yaanze watu 18 wamepoteza maisha ikiwa ni pamoja na polisi mmoja na mamia kujeruhiwa.
Pamoja na risasi za moto na mabomu ya machozi polisi hao wameweka mapipa ya maji na risasi za bandia ili kujaribu kuvunja maandamano hayo.
Waandamanaji wamechukizwa na huduma hafifu za serikali na rushwa.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.