Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:39

Hollande ayashukuru majeshi ya Ufaransa katika mapambano dhidi ya ugaidi


Rais wa Ufaransa, Francois Hollande akikagua kikosi cha Ufaransa kilichopo nchini Iraq.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande akikagua kikosi cha Ufaransa kilichopo nchini Iraq.

Wanajeshi 500 wa Ufaransa wanasadikiwa wanashiriki kampeni ya kuwaondoa wapiganaji wa Islamic State kutoka Mosul ngome yao kuu nchini Iraq.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amewaambia wanajeshi wa Ufaransa ambao wanaisaidia Iraqi kupambana na kundi la Islamic State kwamba juhudi zao zimeweza kuzuia mashambulizi nchini kwao.

“Hatua mnazo zichukua dhidi ya ugaidi hapa Iraq zinazuia vitendo vya kigaidi katika ardhi yetu wenyewe,” Hollande alisema Jumatatu katika kituo cha kupambana na ugaidi nchini humo kilichoko karibu na mji mkuu Baghdad.

Baada ya kuanza ziara yake ya siku moja katika eneo hilo Jumatatu iliyohusisha kuvitembelea vikosi vya Ufaransa, Hollande atakutana na Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, Rais Fuad Masum na spika wa bunge, Salim al-Juburi. Hollande atazuru pia eneo huru la Kurdistan ili kukutana na vikosi vya Ufaransa na viongozi wa serikali.

Televisheni ya taifa nchini Iraq imeripoti kuwa Hollande atafanya mazungumzo juu “ya kuongeza msaada kwa serikali ya Iraq na kuhusu matukio ya hivi karibuni ya vita dhidi ya Daesh,” ambayo ni ufupi wa IS kwa lugha ya Kiarabu.

Ufaransa imefanya maelfu ya mashambulizi ya anga dhidi ya IS nchini Iraq na Syria ikiwa ni sehemu ya majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani katika kupambana na kundi la Islamic State, na imetoa vifaa na mafunzo kwa jeshi la Iraqi.

Vikosi vya Ufaransa, ambavyo ni jumla ya askari 500, inasadikiwa kuwa wanashiriki katika kampeni ya kuwaondosha wapiganaji wa IS kutoka Mosul, ngome yao kuu nchini Iraq.

XS
SM
MD
LG