Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 17:41

Makamanda wa Iraq kushitakiwa.


Waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi upande wa kushoto akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi upande wa kushoto akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi, jumapili amekubaliana na mapendekezo ya tume ya uchunguzi ya kuwafungulia mashitaka makamanda wa kijeshi walioondoka Ramadi mapema mwaka huu wakati mji huo ulipovamiwa na wanmgambo wa ISIS.

Kutekwa kwa mji huo ambao ni mkubwa zaidi katika jimbo la magharibi la Anbar, ulikuwa ni ushindi mkubwa kwa wapiganaji wa Islamic State.Kuchukua udhibiti wa mji mkubwa uliopo kilomita 125 tu kutoka Baghdad pia kuliibua mwaswali magumu kuhusu uwezo wa vikosi vya Iraq.

Kupoteza huko ndio kulimfanya waziri wa ulinzi wa marekani Ash Carter kusema kuwa anashuku ari ya vikosi vya Iraq ambavyo kwa ushirikiano na wapiganaji wanakabiliana na kundi la Islamic State ardhini wakati vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani vikilenga wanamgambo kwa njia ya anga.

Iraq imefanya juhudi za kukomboa maeneo katika jimbo la Anbar, lakini wanamgambo bado wameshikilia maeneo muhimu ukiwemo mji wa Ramadi.

XS
SM
MD
LG