Umoja wa mataifa Jumanne ulionya kuhusu hukumu nyingi za kutisha za kunyonga watu nchini humo baada ya hukumu ya nadra ya Jumatatu ya kuwanyonga wanaume wawili kwa mashtaka ya kuukashifu Uislamu.
Wanaume watatu walinyongwa kwa mashtaka yanayohusiana na dawa za kulevya katika gereza ya Ghezal Hesar katika mji wa Karaj nje ya Teheran, shirika la haki za binadamu lenye makao yake Norway, au IHR, limesema.
Limeongeza kuwa wanaume wengine wanne walinyongwa kwa mashtaka ya ubakaji katika gereza ya Rajai Shahr, ilioko pia katika mji wa Karaj.
Tovuti ya mahakama, Mizan, ilithibitisha kunyongwa kwa watu watatu kwa mashtaka ya dawa za kulevya, ikisema washtakiwa hao walikuwa wanachama wa genge la kusambaza dawa ya kulevya aina ya cocaine. Hakuna taarifa rasmi iliyothibitisha kunyongwa kwa watu wanne kwa mashtaka ya ubakaji.
Shirika la IHR limesema Iran iliwanyonga takriban watu 64 katika siku 12 zilizopita pekee.