Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 16, 2025 Local time: 03:47

Iran yawakamata watu 7 wenye uhusiano na Uingereza kwa kuhusika kwao katika maandamano dhidi ya serikali


Kamanda wa kikosi cha walinzi wa kimapinduzi nchini Iran, Jenerali Hossein Salami
Kamanda wa kikosi cha walinzi wa kimapinduzi nchini Iran, Jenerali Hossein Salami

Taarifa iliyochapishwa na vyombo vya habari vya serikali ya Iran imesema kikosi cha walinzi wa kimapinduzi nchini Iran Jumapili kimewakamata watu saba wenye uhusiano na Uingereza, wakiwemo baadhi ambao wana uraia pacha, kuhusiana na maandamano dhidi ya serikali ambayo yameitikisa nchi hiyo.

Taarifa hiyo imesema “Viongozi wakuu saba wa maandamano ya hivi karibuni wanaohusiana na Uingereza walizuiliwa na idara ya ujasusi ya kikosi cha ulinzi wa mapinduzi ya Iran, wakiwemo watu wawili wenye uraia pacha waliokuwa wakijaribu kuondoka nchini.”

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema imekuwa inatafuta taarifa zaidi kutoka kwa maafisa wa Iran juu ya ripoti za kukamatwa kwa raia wenye uraia wa Uingereza na Iran.

Ripoti ya kukamatwa kwa watu hao inafuatia machafuko yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini tarehe 16 Septemba, mwanamke wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 22, aliyefariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi, ambaye alikamatwa kwa kuvaa mavazi yasiyofaa, chini ya sheria kali za Kiislamu za Iran kuhusu wanawake.

XS
SM
MD
LG