Iran ilithibitisha siku ya Alhamisi kwamba imewahamisha wafungwa wanne wa Kimarekani kwenye kifungo cha nyumbani baada ya mabadilishano ya mabilioni ya dola zilizozuiliwa Korea Kusini jambo ambalo linakuja wakati Tehran kwa miezi kadhaa ikionyesha kuwa iko tayari kubadilishana wafungwa na Washington.
Chini ya makubaliano hayo yaliyosimamiwa na nchi ya tatu raia wa Irani watano waliofungwa nchini Marekani wataachiliwa huru na fedha za Iran zilizozuiliwa nchini Korea Kusini zitatolewa na kuhamishiwa nchini Qatar, Tehran alisema kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Iran -IRNA.
Iran imesema makubaliano hayo na Marekani yalihusisha kati ya dola bilioni 6 na bilioni 7 ambazo zimesitishwa kutokana na vikwazo.
Forum