Trump alisema wiki iliyopita kwamba alituma barua kwa Khamenei akipendekeza mazungumzo ya nyuklia lakini alionya pia kwamba “kuna njia mbili Iran inaweza kushughulikiwa: kijeshi au kuingia mkataba” unaoizuia Tehran kupata silaha za nyuklia.
Mshauri wa kidiplomasia wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Anwar Gargash, alimkabidhi barua hiyo waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araqchi Jumatano.
Mwaka 2018, Trump aliiondoa Marekani kwenye mkataba wa nyuklia wa 2015 na Tehran, huku mataifa yenye nguvu duniani yakiweka tena vikwazo ambavyo vilidhoofisha uchumi wa Iran.
Tehran ilijibu mwaka mmoja baadaye kwa kukiuka mipaka ya mkataba huo wa nyuklia.
Forum