Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 19:54

Iran yadai kubadilishana wafungwa na Marekani


Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian..
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian..

Mwana diplomasia wa juu wa Iran, Jumapili amesema kila kitu kipo tayari kutekeleza mpango uliosimama wa kubadilishana wafungwa na Marekani, ambapo raia wake watatu wanashikiliwa katika magereza ya Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian alizungumza na shirika la habari la serekali la IRINN kwamba wamefikia makubaliano katika siku kadhaa kuhusiana na kubadilishana wafungwa baina ya Iran na Marekani.

Aliongeza kusema kwamba mpango huo ulitiwa saini na kupitishwa japo si moja kwa moja mwaka jana na kilicho baki ni kwamba Marekani inafanya mipango yake ya mwisho ya kiufundi kabla ya kutekeleza jambo hilo.

Mwezi Oktoba, vyombo vya habari vya Iran vieleza kuwepo maafikiano ya kubadilishana wafungwa kati ya Tehran na Washington ikijumuisha kuachilia fedha za Iran nje ya nchi, lakini waziri Amir-Abdollahian, hakugusia hilo Jumapili.

XS
SM
MD
LG