Kwa kubadilishana, Iran siku ya Jumamosi imemwachilia huru Johan Floderus, Msweden ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye taasisi ya kidiplomasia ya Umoja wa Ulaya, pamoja na mtu aliyetambuliwa kama Saeed Azizi na Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson.
Maafisa wa Sweden hawakukubali mpango huo mara moja. Oman ilisimamia mabadilishano hayo, Shirika la Habari la Oman liliripoti. Televisheni ya taifa ya Iran iliripoti kuwa Nouri alikuwa tayari amekwishaachiliwa huru na anarejea Tehran. Mwaka 2022, Mahakama ya Wilaya ya Stockholm ilimhukumu Nouri kifungo cha maisha jela kwa kuhusika kwake katika mauaji hayo.
Forum