Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 26, 2026 Local time: 12:18

Iran imefanya majaribio ya kufyatua makombora ya masafa marefu

Vyombo vya habari vya Iran vimesema makombora mawili ya Qadr H yalifyetuliwa yakilenga shabaha zilizokuwa na umbali wa kilomita 1,400.

Iran inasema imefanya majaribio mawili zaidi ya kufyetua makombora ya masafa marefu , siku moja baada ya Marekani kukosoa mfululizo wa majaribio ambayo Iran ilielezea kama uwezo wake wa kukabiliana na uchokozi.

Vyombo vya habari vya Iran vimesema makombora mawili ya Qadr H yalifyetuliwa leo yakilenga shabaha zilizokuwa na umbali wa kilomita 1,400.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema jana kwamba ilipanga kuliomba baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutathmini hali na kushinikiza kupatikana majibu sahihi.

This item is part of
XS
SM
MD
LG