Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:26

Iran inawanyonga waandamanaji


Maafisa wa polisi wa Iran wakijitayarisha kumnyonga Mohammad Ali Sarvari, mjini Tehran
Maafisa wa polisi wa Iran wakijitayarisha kumnyonga Mohammad Ali Sarvari, mjini Tehran

Serikali ya Iran imetangaza kumnyonga mtu wa pili ambaye aliyehusishwa na maandamano ambayo yamekumba sehemu zote za nchi hiyo kuanzia mwezi Septemba, kufuatia kifo cha mwanamke aliyekuwa anazuiliwa na polisi kwa kutofunika nywele zake kwa hijab.

Shirika la habari la Mizan, ambalo linamilikiwa na wizara ya sheria ya Iran, limesema kwamba Majidreza Rahnavard, amenyongwa kwenye krane ya ujenzi, katika mji wa Mashhad, likiwa ni onyo kwa wengine wanaoshiriki maandamano hayo.

Rahnavard alishutumiwa kwa kuwachoma kisu hadi kufa maafisa wawili wa usalama mwezi uliopita, baada ya kukasirishwa na ripoti kwamba maafisa wa usalama walikuwa wakiwaua waandamanaji.

Maandamano yalianza kote nchini Iran baada ya Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22, kufariki akiwa mikononi mwa polisi.

Wanaharakati wamesema kwamba Iran imewahukumu kifo darzeni ya watu baada ya kesi zao kusikilizwa bila ya kufuatiliwa na umma wala waandishi wa habari.

Wau 488 wameuawa katika maandamano ya Iran ambayo yameingia mwezi wa tatu. Watetezi wa haki za kibinadamu nchini Iran wamesema kwamba watu 18,200 wamekamatwa na kuzuiliwa.

Mtu wa kwanza aliyehukumiwa kifo kutokana na maandamano hayo, alinyongwa wiki iliyopita.

XS
SM
MD
LG