Taarifa ya idara ya mahakama ya Iran imesema kwamba Mohammad Mahdi Karami na Seyyed Mohammad Hossein wamenyongwa kwa kumuua afisa wa usalama wakati wa maandamano.
Maandamano yamekuwa yakifanyika kote nchini Iran tangu kifo cha mwanamke aliyekuwa amezuiliwa na polisi kwa kukosa kuvaa hijab inavyotakiwa.
Jumla ya waandamanaji wanne wameuawa kwa kunyongwa nchini Iran tangu maandamano ya kuipinga serikali kuanza mwezi Septemba.