Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:36

Iran ilinyonga zaidi ya watu 100 miezi mitatu ya kwanza ya 2022-Ripoti ya UN


Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mahojiano kwenye makao makuu ya UN, mjini New York, January 20, 2022. Picha ya AP
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mahojiano kwenye makao makuu ya UN, mjini New York, January 20, 2022. Picha ya AP

Iran iliwanyonga zaidi ya watu 100 katika miezi mitatu ya kwanza ya 2022, hali ya kutisha ambayo inazidi kuongezeka, kulingana na ripoti ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres iliyowasilishwa Jumanne.

Akizungumza mbele ya Baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa mjini Geneva, naibu mkuu wa Umoja wa mataifa wa masuala ya haki za binadamu Nada Al-Nashif aliwasilisha ripoti ya hivi karibuni ya Guterres kuhusu Iran, akisema kwamba hukumu za kunyonga watu nchini humo zimeongezeka.

“Wakati watu 260 walinyongwa mwaka wa 2020, takriban watu 301 walinyongwa mwaka wa 2021, wakiwemo wanawake 14, amesema, akiongeza kuwa hali hiyo imeendelea kuongezeka mwaka huu.

Kati ya Januari 1 na Machi 20, amesema “takriban watu 105 walinyongwa”, wengi wao wakiwa ni kutoka kwenye makundi ya walio wachache.

Ripoti ya Guterres ilibaini kwa wasiwasi mkubwa ongezeko la hukumu za kunyonga kwa ajili ya uhalifu mdogo, yakiwemo makosa yanayohusiana na dawa za kulevya, Nashif amesema.

“Adhabu ya kifo inaendelea kutolewa kwa misingi ya mashtaka yasiyofikia uhalifu mkubwa, na kwa njia zisizolingana na vigezo vya kesi za haki,” ameliambia Baraza la Umoja wa mataifa la haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG