Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 25, 2020 Local time: 14:14

Iran yaituhumu Marekani kwa kuendeleza vitisho


Rais Hassan Rouhani

Rais wa Iran, Hassan Rouhani amesema leo Jumanne kwamba nchi yake inapendelea kuendelea na mkataba wa kimataifa wa mwaka 2015 juu ya program yake ya nyuklia.

Lakini ameeleza kuwa kama Marekani inaendeleza vitisho na vikwazo, basi Iran haraka itaweza kurejea kwenye harakati zake za nyuklia hadi kufikia kiwango cha juu kabla ya mkataba kuanza kazi.

Akizungumza na wabunge kwenye hotuba iliyotangazwa na televisheni, Rouhani alisema Marekani si mshirika mzuri.

“Wale ambao wanajaribu kurudi kwenye lugha za vitisho na vikwazo ni wafungwa wa mitazamo yao ya nyuma,” Rouhani alisema. wanajinyima fursa ya amani.

Iran inapinga vikwazo vipya, ambavyo rais wa Marekani Donald trump alitia saini mwanzoni mwa mwezi huu dhidi ya watu waliohusika na program ya makombora ya masafa marefu ya iran na kikosi maalum cha ulinzi cha Revolutionary Guard.

Hatua hiyo ya Trump imekuja ikiwa ni ujumbe wa kuitaka Iran isiendelee na majaribio ya makombora ya masafa ya marefu.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG