Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 02:27

IOM yakadiria wakimbizi elfu 50 wamekufa wakitafuta maisha bora kwingineko


Desemba 18 ni siku ya kimataifa ya wahamiaji ambapo umoja wa mataifa umetenga maadhimisho haya kukumbuka michango ya mamia ya wahamiaji ambao wamekabiliwa na changamoto za kuondoka katika makazi yao kutafuta maisha bora kwingineko.

Mwaka huu maadhimisho haya yanafanyika wakati ambapo nchi nyingi za ulaya zimefunga milango yake kupokea wakimbizi na wahamiaji wanaokabiliwa na changamoto za kiuchumi kutoka Afghanistan , mashariki ya kati, na Afrika.

Yanafanyika wakati idadi kubwa ya wahamiaji wanajaribu kuvuka mpaka kuingia Amerika ya kusini pia. Umoja wa mataifa unasema watu hawaondoki nyumbani kwao kwa mapenzi yao.

Inasema karibu wahamiaji wote duniani takriban milioni 280 wanalazimika kuondoka kutokana na ghasia, mauaji, umasiki mkubwa, na ongezeko la mabadiliko ya hali ya hewa.

Wahamiaji wengi wasiokuwa na vibali vya kisheria kuingia kwenye nchi nyingine, wanapitia njia hatari kwenye nchi mbalimbali wakitafuta hati ya ukaazi.

Wengi wanauzwa, kunyanyaswa, na wanakufa wakiwa njiani shirika la kimataifa la wahamiaji la IOM linakadiria kwamba takriban wakimbizi elfu 50 wamekufa na wengine maelfu hawajulikani walipo kwa takriban miaka nane iliyopita.

Mkurugenzi mkuu wa IOM Antonio Vitorino amesema dunia imeshindwa kulinda watu wengi waliojikuta katika hali ngumu.

Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus ameunga mkono taarifa hiyo . Anasema nchi zina fursa ya kisheria kuwasaidia wale walio na taabu na kutoa huduma msingi za afya na ulinzi kwao. Umoja wa kimataifa unasema haki za wahamiaji ni za kibinadabu, na nilazima ziheshimiwe bila kutengwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG