Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 06:34

IOM inasema wa Afrika 6,600 wamekufa miaka mitano iliyopita


Taasisi ya kimataifa ya wahamiaji-IOM
Taasisi ya kimataifa ya wahamiaji-IOM

Taasisi hiyo inaripoti vifo vingi vilivyorekodiwa vimetokea kwenye jangwa la Sahara, Kaskazini mwa Niger, Kusini mwa Libya na Kaskazini mwa Sudan ambapo wahamiaji wanatumia njia hizi kufika Libya, kuingia ulaya wakiwa na matumaini ya kupata maisha bora.

Rekodi mpya iliyotolewa na taasisi ya kimataifa kwa wahamiaji-IOM iligundua zaidi ya wa-Afrika 6,600 wamekufa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wengi wao wakiwa wanavuka jangwa la Sahara kuelekea ulaya. Hata hivyo utafiti unaeleza kwamba idadi hii ya watu ni kidokezo tu.

Mwaka 2018 pekee mamia ya watu walioshuhudia wamethibitisha takribani vifo 1,400 vya wahamiaji kwenye bara la Afrika. Lakini watafiti wanasema idadi hii inawakilisha kiasi kidogo tu cha idadi jumla ya vifo vya watu wanaohama barani Afrika.

Taasisi ya kimataifa ya wahamiaji-IOM inaripoti vifo vingi vilivyorekodiwa vimetokea kwenye jangwa la Sahara, Kaskazini mwa Niger, Kusini mwa Libya na Kaskazini mwa Sudan. IOM inasema wahamiaji wanatumia njia hizi kufika Libya, kuingia ulaya na wakiwa na matumaini ya kupata maisha bora.

Msemaji wa IOM, Joel Millman alisema njia za wahamiaji zinatumiwa na wafanyabiashara wa magendo na wasafirishaji haramu watu ambao wanatumia fursa hii ya kufanya harakati zao kwa wahamiaji wa Afrika. Alisema sababu kuu ya vifo vya wahamiaji kurekodiwa huko Afrika inaonesha kwamba vingi vinaweza kuzuilika.Njaa, ukosefu wa maji mwilini, unyanyasaji wa mwili, magonjwa na ukosefu wa fursa ya madawa ni sababu za vifo vya mara kwa mara inayoelezewa kwa wahamiaji ambao wanaripotiwa kufa wakiwa njiani ndani ya bara la Afrika. Ikihusishwa na biashara magendo ya binadamu na usafirishaji haramu wa watu kunaweza kuwaweka watu katika hali hatarishi ambapo kuna taasisi ndogo ya kuwalinda wenyewe na kuwaacha wasafiri wenzao wakinyanyasika”.

Wakati vifo vingi vinaelezewa kuwa vya vijana wanaume, Millman aliiambia Sauti ya Amerika-VOA mamia ya wanawake na watoto pia ni miongoni mwa waathirika. Alisema utafiti ambao unahusisha vifo vya wahamiaji unaeleza kwamba msaada kidogo unatolewa kwa watu ambao wamenusurika na safari hiyo mbaya.

Alisema watu ambao wameshuhudia wasafiri wenzao wakifariki wapo kwenye msongo mbaya wa mawazo. Alisema wanashuhudia msongo wa kiakili lakini wanapatiwa msaada kidogo wa kuwaponya kutokana na matukio ya kutisha wanayoyaona.

XS
SM
MD
LG