Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:43

Indonesia kunyonga wasafirisha dawa za kulevya


Moja ya gereza kisiwani Bali, Indonesia
Moja ya gereza kisiwani Bali, Indonesia

Wasafirisha dawa za kulevya wawili raia wa Australia walichukuliwa kutoka gereza la Bali, Jumatano na kupelekwa katika kisiwa ambacho watanyongwa nchini Indonesia.

Andrew Chan (31), na Myuran Sukumaran (33), ambao walikuwa gerezani miaka kumi iliyopita waliambatana na raia wa Nigeria, Raheem Agbaje Salami (45), aliyezaliwa Cordova, Hispania, na raia wa Ufilipino, Mary Jane Fiesta Veloso (30).

Wote kwa pamoja watasafirishwa mpaka katika kisiwa cha Nasakambangan, ambako wanatarajiwa kukabiliwa na kikosi cha wapiga risasi mnamo siku zijazo.

Wafungwa wengine watano raia wa kigeni wawili kutoka Nigeria, Brazil, Ufaransa na Ghana pia watanyongwa katika gereza la kisiwani, nje ya kisiwa kikuu cha Indonesia cha Java.

XS
SM
MD
LG