Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:43

India yatangaza amri ya kutotoka nje Kashmir


Maafisa wa usalama wa jimbo la Kashmir linalotawaliwa na India watangaza amri ya kutotoka nje siku moja baada ya maandamano kupinga utawala wa New Delhi.

Wanajeshi katika jimbo la Kshamiri linalotawaliwa na India wanapiga doria katika mitaa ya Srinagar, mji mkuu wa jimbo hilo, wakiweka vizuizi vya sinyenge kufunga viwanja vya umaa.

Amri ya kutotoka nje ilitangazwa Jumapili, siku moja baada ya waandamanaji kutia moto majengo ya serikali wakati wa malalamiko dhidi ya utawala wa New Delhi.

Polisi wamemtuhumu kiongozi mkuu wa makundi yanayotaka kujitenga kwa jimbo hilo, Mirwaiz Umar Farooq kwa kuchochea ghasia hizo. Farooq anakanusha tuhuma hizo. Malefu na maelfu ya watu waliandamana mjini Srinigar siku ya Jumamosi mara baada ya sala ya Idd El Fitri.

Kashmir imekumbwa na malalamiko ya karibu miezi mitatu sasa dhidi ya utawala wa India. Takriban waandamanaji 69 wameuwawa katika ghasia, wengi wao wamefariki baada ya polisi kufyetua risasi dhidi ya umati wa watu walokua wanbawatupia mawe.

Chuki dhidi ya utawala wa India ina nguvu katika jimbo hilo lenye waislamu wengi, na makundi yanayotaka kujitenga kwa Kashmri yamepigania uhuru kwa miongo kadha kutoka India au kujiunga na Pakistan yenye waislamu wengi.

XS
SM
MD
LG