Maandamano hayo yamepelekea shinkizo la kufanyika mazungumzo mapya.
Wakulima hao, wengi wao kutoka jimbo la kaskazini la Punjab, wamekuwa wakitaka bei za mazao kuongezwa, sawa na kuwepo sheria inayosimamia mazao yao.
Idadi kubwa ya wapiga kura wanaomuunga mkono waziri mkuu Narendra Modi ni wakulima, na Modi anajaribu kutimiza matakwa yao kabla ya uchaguzi wa mwezi May.
Waziri wa kilimo Arjun Munda ameandika ujumbe kwenye mtandao wa X kwamba serikali iko tayari kwa mazungumzo na wakulima na kwamba amewaalika kiongozi wao kwa mazungumzo zaidi.
Forum