Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 11:16

India na Japan kuzidisha ushirikiano wa kiulinzi


Waziri wa ulinzi wa India, Rajnath Singh, na waziri wa ulinzi wa Japan, Yasukazu Hamada, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wa pamoja katika wizara ya ulinzi ya Japan, Tokyo, Septemba 8, 2022.

India, na Japan, Alhamisi zimesema zitaimarisha ushirikiano wa kiulinzi ambapo New Delhi, imekaribisha uwekezaji wa viwanda vya Japan na mataifa yote mawili yanapanga mazoezi ya pamoja yakihusisha vikosi vyao.

Waziri wa ulinzi wa India, Rajnath Singh, alifanya mazungumzo na Tokyo, na mwenzake Yasukazu Hamada, na baadaye wote wawili watajiunga na mawaziri wao wa mambo ya nje katika mazungumzo zaidi ya siku mbili.

Mawaziri hao wawili wamekubaliana kufanyika kwa mapema kwa ufunguzi wa mazoezi ya kijeshi kutafungua njia kwa ushirikiano mkubwa zaidi na operesheni za pamoja za majeshi ya anga ya mataifa hayo mawili.

India kama ilivyo kwa Japan, itaboresha jeshi lake katika kile inachokiona kama kuongezeka kwa tishio la kiusalama ikijumuisha jirani yake China.

XS
SM
MD
LG