Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 20:20

India kuongeza ushirikiano na Russia


India itaongeza ushirikiano na Russia na kuendelea kununua mafuta kutoka Moscow, amesema waziri wa mambo ya nje wa India, akigusia kuingizwa kwa mafuta ghafi ambayo hayaku jumuishwa kwamba yana maslahi kwao.

Waziri wa mambo ya nje Subrahmanyam Jaishankar, amesema katika ziara yake ya Moscow kwamba ikiwa ni taifa la tatu kwa ununuzi wa kiwango kikubwa cha mafuta, ni jukumu lao kuhakikisha wanunuzi wa India wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kupata mafuta ya bei nzuri linapokuja soko la kimataifa.

Alitoa kauli hiyo baada ya kukutana na mwenzake waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergey Lavrov siku ya Jumanne.

Ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya Russia toka kuzuka kwa mgogoro wa Ukraine, waziri huyo wa India amehakikishia ushirika wa siku nyingi wa New Delhi na Moscow kuwa ni wa kipekee na madhubuti.

XS
SM
MD
LG