Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 14:51

Mkanyagano wauwa 27 India


Mahujaji wakusanyika kuhudhuria sherehe za Maha Pushkararu, India
Mahujaji wakusanyika kuhudhuria sherehe za Maha Pushkararu, India

Mamlaka ya India yanasema takriban watu 27 wameuwawa baada ya makanyagano kwenye ukingo wa mto ambako mahujaji walikuwa wamekusanyika katika sherehe za kihindu za kuoga.

Mkanyagano huo umetokea jumanne kwenye jimbo la kusini la Andhra Pradesh wakati maelfu ya watu walipokimbia kuoga kwenye mto Godaravi. Zaidi ya darzeni mbili wengine wamejeruhiwa kwenye mkanyagano huo. Waziri mkuu Narendra Modi ametoa taarifa kupitia akaunti yake ya tweeter akisema amesikitishwa na tukio hilo.

Waziri kiongozi wa Andhra Pradesh amesema kuwa serikali italipa fidia ya dola 15,570 kwa waathirika wa mkasa huo. Jumanne ndiyo ilikuwa mwanzo wa sherehe za Maha Pushkararu wakati mamilioni ya watu wakitarajiwa kufanya hija kwenye mto Godavari wakifanya ibada kwa siku 12 zijazo.

Mikanyagano ni matukio ya kawaida nchini India wakati wa sherehe za kidini wakati ambapo mamilioni ya watu hukusanyika katika maeneo madogo huku idadi yao ikiwaelemea maafisa wa usalama kutoa ulinzi.

XS
SM
MD
LG