Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 05:25

Imran Khan asema mashitaka ya ugaidi dhidi yake yamechochewa kisiasa


Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters huko Islamabad. REUTERS/Saiyna Bashir.
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters huko Islamabad. REUTERS/Saiyna Bashir.

Mahakama moja ya Pakistan siku ya Alhamisi iliongeza muda wa ulinzi wa waziri mkuu wa zamani Imran Khan dhidi ya kukamatwa hadi mwisho wa mwezi, maafisa walisema, baada ya polisi kuwasilisha mashtaka ya ugaidi dhidi ya kiongozi maarufu wa upinzani nchini humo.

Mahakama ilimlinda Khan dhidi ya kukamatwa hadi Septemba mosi kwa tuhuma kwamba wakati wa hotuba mwishoni mwa juma, aliwatishia maafisa wa polisi na hakimu mwanamke. Matukio hayo kabla ya ahueni ya mahakama kwa Khan yalizua hofu ya makabiliano makali kati ya polisi na Khan, ambaye anaongoza mikutano ya hadhara na kutaka uchaguzi wa haraka baada ya kuondolewa madarakani.

Serikali inasema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa mwaka ujao.

Siku ya Alhamisi, Khan aliwaambia wanahabari nje ya mahakama kwamba hakuwahi kutishia mtu yeyote.

Alisema mashtaka ya ugaidi dhidi yake yamechochewa kisiasa na kwamba serikali ya Waziri Mkuu Shahbaz Sharif inahofia umaarufu wa Khan unaoongezeka.

XS
SM
MD
LG