Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 12:24

IMF yaidhinisha mkopo wa dola bilioni 3.4 kwa Ethiopia


Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva
Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva

Ethiopia yenye matatizo ya fedha Jumatatu ilipunguza viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni kama sehemu ya mpango mpana wa mageuzi ya kiuchumi, huku shirika la kimataifa la fedha (IMF) likiidhinisha mkopo kwa taifa hilo ambalo linatafuta mabilioni ya dola, ili kujikwamua kiuchumi.

Thamani ya sarafu ya ndani, birr, ilishuka kwa karibu asilimia 30 baada ya hatua ya benki kuu ya taifa.

“Mageuzi haya yanaleta ushindani unaotegemea soko la kiwango cha ubadilishaji wa fedha na kushughulikia mapungufu ya muda mrefu ndani ya uchumi wa Ethiopia,” Benki ya Taifa ya Ethiopia (NBE) ilisema katika taarifa.

Nchi hiyo ya pili yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika ina matumaini ya kupata angalau dola bilioni 10.5 kutoka kwa wakopeshaji wa nje ikiwemo IMF, lakini mazungumzo yamechukua muda mrefu na yamekuwa magumu.

Bodi ya IMF Jumatatu iliidhinisha mpango wa miaka minne wa dola bilioni 3.4 kuunga mkono mageuzi hayo, huku dola bilioni 1 zikitolewa mara moja.

“Huu ni wakati wa kihistoria kwa Ethiopia, na mkopo huu ni ushahidi wa “dhamira kubwa ya nchi hiyo katika kuleta mageuzi”, Mkurugenzi Mkuu wa IMF Kristalina Georgieva alisema katika taarifa.

Forum

XS
SM
MD
LG