Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 19:29

ILO yasema kwamba Covid ingali imeumiza mataifa kiuchumi


ILO logo, International Labor Organization, graphic element on black
ILO logo, International Labor Organization, graphic element on black

Takwimu mpya kutoka kwa shirika la Umoja wa taifa la wafanyakazi ILO zinaonyesha kwamba sekta ya ajira imekuwa na kasi ndogo katika kurejea kwenye hali ya kawaida baada ya janga la Covid 19, wakati mataifa yanayoendelea yakisemekana kuathirika zaidi yakilingaishwa na yale yalioendelea.

Wachumi wa ILO wamekuwa wakifautilia athari za covid-19 kwenye sekta ya ajira kote ulimwenguni tangu Machi mwaka uliyopita. Mwanzoni mwa mwaka huu walitabiri ukuaji mdogo kwenye sekta hiyo. Hata hivyo wanasema kwamba hilo halikufanyika kutokana na wimbi jipya la maambukizi ambalo lilipunguza kasi ya ukuaji wa uchumi kama ilivyotarajiwa.

Kutokana na takwimu hizo, ILO inasema kwamba jumla ya masaa ya yaliotumiwa na wafanyakazi kote ulimwenguni mwaka huu yatashuka kwa asilimia 4.3 yakilinganishwa na miaka kabla janga halijatokea. Asilimia hiyo ni sawa na kupotea kwa ajira milioni 125 kote ulimwenguni.

Mkuu wa ILO,Guy Ryder alisema kwamba wasiwasi mkubwa ulioko ni kutokana ya tofauti ya kasi ya ukuaji wa uchumi kati ya mataifa masikini na matajiri. "Hilo ni wazi kwa kuwa mataifa tajiri mwaka huu yameweza kujikwamua kwa kiasi fulani wakati yale masikini yakiendelea kuathiriwa vibaya na janga hilo. Janga hilo limeongeza ukosefu wa usawa baina ya mataifa na pia ndani ya mataifa." Ryder analaumu hali iliyoko kwa ukosefu wa usawa katika usambazaji wa chanjo za covid pamoja na utoaji wa misaada ya fedha ili kujikuamua kiuchumi.

Amesema kwamba kasi ya kila taifa ya kujikwamua inategemea pakubwa uwezo wa kutoa chanjo kwa watu wake. Ameongeza kusema pia kwamba inategemea uwezo wa kila taifa wa kutoa misaada ya kifedha ili kulinda ajira za watu pamoja na biashara zilizoathiriwa na janga hilo.

ILO limeongeza kusema kwamba matumaini ya kuinuka kiuchumi kwa mataifa mengi ndani ya miezi iliyobaki mwaka huu bado ni hafifu. Ryder ameongeza kusema kwamba hakuna taifa linaloweza kujikwamua kutoka kwenye janga hilo peke yake. Anasema njia pekee ni kupitia ushirikiano

XS
SM
MD
LG