Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 09:53

Ikulu ya Marekani: Korea Kaskazini inaipatia Russia silaha kwa siri


Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa, John Kirby akizungumza katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari huko Ikulu mjini Washington. (REUTERS)
Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa, John Kirby akizungumza katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari huko Ikulu mjini Washington. (REUTERS)

Ikulu ya Marekani ilisema Jumatano kwamba Korea Kaskazini inaipatia Russia silaha kwa siri kwa ajili ya vita vya Ukraine.

Hi ikiwa ni ishara nyingine ya kutia wasiwasi, wachambuzi wanasema, kwamba mzozo huu unazidi kuwa mgumu na hatari kwa raia wa Ukraine.

Habari zetu zinaonyesha kuwa Korea inasambaza silaha kwa vita vya Russia nchini Ukraine kwa siri idadi kubwa ya makombora ya mizinga, huku ikitatanisha mahali halisi ambapo silaha hizo zinapelekwa kwa kujaribu kufanya ionekane kana kwamba zinatumwa katika nchi za Mashariki ya Kati au Afrika Kaskazini,” John Kirby, Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa, aliwaambia waandishi wa habari

Kirby aliongeza kuwa makombora ambayo Korea Kaskazini inatuma "hayatabadilisha mkondo wa vita," na kwamba msaada wa usalama wa Marekani kwa Ukraine utaendelea na kukabiliana na changamoto mpya.

XS
SM
MD
LG